Latest News and Events

Profesa Joyce Ndalichako Apongeza Juhudi Zinazofanywa na Chuo Kikuu Cha Iringa

ProfNdalichako

Waziri wa Sayansi, Tekinologia na Mafunzo ya Ufundi - Prof. Joyce Ndalichako apongeza juhudi zinazofanywa na Chuo Kikuu cha Iringa katika kutoa elimu kwa nadharia na vitendo. 

Pongezi hizo alizitoa leo tarehe 01/06/2019 chuoni hapa alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya kitivo cha sayansi na Elimu.

Katika sherehe hizo waziri alifanikiwa kutembelea na kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na wahadhiri pamoja na wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Iringa na kushuhudia jinsi ambavyo Elimu inayotolewa Chuoni hapa inavyomjengea uwezo mkubwa mwanafunzi wa kuweza kujiajiri bila kutegemea sana kuajiriwa kwani wanafunzi hawa hawasomi nadharia tu bali pia wanafanya kwa vitendo yale wanayofundishwa.

Mfano mzuri ni pale waziri alipotembelea kiota hub ambapo wanafunzi wetu washahada ya masoko na ujasiriamali kwa vitendo (Bachelor of Applied Marketing and Entrepreneurship-BAME) walipomuonyesha bidhaa walizotengeneza na kufanikiwa kuziuza, pia walipoonyesha uwezo wao wa kubuni na kusimamia miradi.

Katika kujibu kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi hao mheshimiwa waziri amekiri kuzipokea changamoto hizo na ameahidi kuzifanyia kazi kwa kushirikiana na uongozi wa chuo pamoja na wizara zinazohusika.

Prof.Ndalichako ametoa Rai kwa wanafunzi wote kusoma kwa bidii na kujiepusha na makundi yasiyofaa,huku akiwakumbusha wanafunzi kuhusu janga la Ukimwi.

 

Connect with us

University of Iringa, P.O Box 200, Iringa, Tanzania

  Tel: +255 (0) 26 2720900

  Fax: +255 (0) 26 2720904

  E-Mail: uoi@uoi.ac.tz

Search